` WACHEZAJI WAKE KWA KUMWANDIKIA HISTORIA SAFI
MCHEKI `MNYAMA` CRISTIANO DOS SANTOS AVEIRO RONALDO AKISHANGILIA BAO LAKE KWA KUTUNISHA KIFUA....HADI RAHAAA!
Ronaldo akishangilia bao lake la penati katika dakika za nyongeza uwanja wa Stadium of Light mjini Lisbon
NGOMA DAKIKA 120, REAL MADRID YAICHAPA ATLETICO MADRID 4-1 NA KUTWAA `DEBE` LA 10 LA UEFA, BALE NI KIBOKO, APIGA BAO MUHIMU MNO..
Bale akiwa na bendera ya nchi yake wakati akishangilia ushindi wa Real Madrid.
Nahodha Iker Casillas akinyanyua kombe
Ronaldo akinyanyua kombe mjini Lisbon baada ya Real kushinda dakika za nyongeza
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia ubingwa wao wa 10
Imechapishwa Mei 25, 2014, saa 7:00 usiku
HATIMAYE Gareth Bale ameisaidia Real Madrid kutumiza ndoto za `La Decima` baada ya kutwaa ndoo ya 10 ya UEFA kufuatia ushindi wa dakika za nyongeza katika mchezo wa fainali dhidi ya majirani zao Atletico Madrid.
Alizaliwa Wales, alikulia Southampton na kung`ara Tottenham, nyota huyo mwenye miaka 24 ameendelea kuonesha kuwa Real Madrid hawakukosea kumsajili kwa rekodi ya dunia baada ya kufunga bao ambalo limeandikwa katika historia ya klabu.
Bale alionekana kutokuwa makini kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi za kufunga, lakini aliendeleza rekodi nzuri ya msimu wake wa kwanza Real Madrid baada ya kuifungia bao la pili katika dakika za nyongeza, kabla ya vijana hao wa Carlo Ancelotti kushinda kwa mabao 4-1.
Kikosi cha Real Madrid:
Casillas, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao (Marcelo 59),
Modric, Khedira (Isco 59), Di Maria, Bale, Benzema (Morata 79), Ronaldo.
Wachezaji wa akiba: Diego Lopez, Pepe, Arbeloa, Illarramendi.
Waliopata kadi za njano: Ramos, Khedira, Marcelo, Ronaldo, Varane.
Waliofunga magoli. Ramos 90, Bale 110, Marcelo 118, Ronaldo 120.
Kikosi cha Atletico Madrid: Courtois,
Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis (Alderweireld 83), Raul Garcia
(Sosa 66), Gabi, Tiago, Koke, Villa, Diego Costa (Adrian 9).
Wachezaji wa akiba: Aranzubia, Mario Suarez, Rodriguez, Diego.
Mfungaji wa Goli: Godin 36.
Walioneshwa kadi nyekundu: Garcia, Miranda, Villa, Juanfran, Gabi, Koke, Godin.
Mwamuzi: Bjorn Kuipers (Holland)
0 comments:
Post a Comment