KWA SABABU WALIZOTOA SASA ZINAFANANA NA ZA UHOLANZI
HISPANI wametakiwa kubadilisha jezi zao Kombe la Dunia baada ya FIFA kuamua jezi zao za sasa zinafanana na za Uholanzi.
Wasambazaji
wa nguo za Hispania, Adidas wamesema jana kwamba FIFA wameagiza
Hispania ichapishe jezi ya tatu- nyeupe - ambayo wataitumia katika
mchezo wao wa kwanza na Brazil.
Mgongngano:
Jezi mpya za Hispania, znazoonyeshwa na Andres Iniesta, Xabi Alonso na
Pedro (kushoto) zinafanana sana na za Uholanzi
FIFA intaka
kila timu iwe na aina mbili za jezi katika kila pea kwa ajili ya
mashindano hayo - moja yenye range nyepesi na nyingine nzito.
Jezi
za Hispania ni nyekundu kwa mechi za nyumbani na nyeusi kwa mechi za
ugenini, wakati Uholanzi kwa kawaida huvaa range ya chungwa nyumbani na
bluu ugenini waliyopanga kuvaa dhidi ya Hispania wakati timu hizo
zitakapokutana katika mechi za Kundi B Juni 13.
0 comments:
Post a Comment