Mahmoud Ahmad Arusha
Wananchi waishio kata ya
Elkiding’a wilaya ya Arusha wameshinda kesi kwenye mahakama kuu ya mkoa
wa Arusha dhidi ya Halmashauri ya wilaya hiyo leo(jana) jijini hapa
mbele ya jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha.
Kesi hiyo no.18 ya mwaka 2013
waliokuwa wakiilalamikia halmashauri ya Arusha kuvunja nyumba zao pamoja
na kung’oa miti iliyokuwa pembezoni mwa barabara ya Mianzini hadi
kijiji cha Timbolo ilizua furaha na machozi ya furaha kwa wananchi hao
mahakamani hapo.
Akisoma hukumu hiyo Jaji
mfawidhi Bi Fatuma Masengi aliitaka halmashauri hiyo kuleta watathmini
ndani ya miezi mitatu kupitia uharibufu waliofanya wa kuvunja nyumba
hizo za wananchi waliokuwa pembezoni mwa barabara hiyo.
Wakiwa na nyuso za furaha
wananchi hao zaidi ya 43 mmoja wa viongozi ambao walikuwa wakiifuatilia
kesi hiyo Fanuel Taitus alisema kuwa haki imetendeka na imeonyesha kuwa
mahakama hiyo chini ya majaji wanawake inaendeshwa kwa mujibu wa sheria
za nchi na wanaimani nao.
Taitus Akatanabaisha kuwa
halmashauri hiyo ya Arusha zamani Arumeru ilishindwa kukaa nao kujua na
kutathmini mali zao ili waweze kufidiwa na kuwa walitumia mabavu kwani
wao pia ni wadau wamaendeleo hivyo hawakatai maendeleo ila walitaka haki
itendeke pale maendeleo yanaposogea kwenye vijiji vyao.
“Sisi sasa tunangoja utekelezaji
wa hukumu ndani ya miezi mitatu waliopewa halmshauri kuleta watathmini
kuja kukagua ilituweze kupata haki yetu kwani pia maendeleo ni yetu sote
ila tumekosa makazi na sehemu za kwenda kuishi”alisema Taitus.
Juhudi za kumpata mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Arusha Phidelis Lumato zilishindikana kwani
alikuwa nje ya ofisi na simu yake ilikuwa ikiita bila majibu na juhudi
zinaendelea ilikupata ufafanuzi wa hukumu ya mahakama.
0 comments:
Post a Comment