MSAFARA
wa watu 30 wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
unaojumuisha wachezaji, benchi la ufundi umefungiwa vyumba vya hoteli
mjini Harare Zimbabwe, ambako wapo kwa ajili ya mchezo na wenyeji kesho
hatua za awali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Stars
imefikia katika hoteli ya Best City Lodge mjini Harare na baada ya
wachezaji kurejea kutoka mazoezini, wakanyimwa funguo za kuingia
vyumbani, wakambiwa hawajalipiwa malazi hapo.
Wakati huu wachezaji wakiwa eneo la mapekezi wameketi, viongozi wa TFF wanahaha kutatua tatizo hilo.
Stars itacheza na Zimbabwe Jumapili mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
Katika mchezo wa kwanza, Tanzania ilishinda bao 1-0 wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Jumapili Uwanja wa Taifa wa Harare, itahitaji sare ili kusonga mbele.
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mapokezi baada ya kuzuiliwa kuingia vyumbani |
Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto na wachezaji wenzake wakiwa mapokezi |
Wakati huu wachezaji wakiwa eneo la mapekezi wameketi, viongozi wa TFF wanahaha kutatua tatizo hilo.
Stars itacheza na Zimbabwe Jumapili mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
Katika mchezo wa kwanza, Tanzania ilishinda bao 1-0 wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Jumapili Uwanja wa Taifa wa Harare, itahitaji sare ili kusonga mbele.
Na Mwandishi Wetu, HARARE
0 comments:
Post a Comment