Amepumua: Arsene Wenger akishangilia baada ya kumaliza ukame wa miaka 9 bila kombe mwezi huu baada ya kutwaa taji la FA.
Chagamoto kubwa: Wenger kwa sasa anahitaji kupeleka nguvu za FA katika michuano ya ligi kuu.
Imechapishwa Mei 30, 2014, saa 9:56 alasiri
ASERNE
Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Asernal siku chache
zijazo baada ya kukubaliana na vipengelea vya mkataba huo ambao
utamuweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2017.
Wenger
alimaliza hofu ya kuondoka klabuni hapo majira ya kiangazi mwaka huu
baada ya kufuta ukame wa miaka 9 bila kombe kufuatia kutwaa `ndoo` ya
kombe la FA.
Kulikuwa
na hoja kuwa kama kocha huyo mwenye miaka 64 angeshindwa kumaliza ukame
wa miaka 9 bila kombe Emirates basi angefutiwa kazi yake, lakini Wenger
alionesha maarifa yake Wembley baada ya kuitwanga 3-2 Hull na
kujihakikishia maisha London kaskazini.
Arsenal wamempatia Wenger mkataba wenye thamani ya paundi milioni 24 na paundi milioni 100 kwa ajili ya usajili.
MPENJA BLOG kupitia mtandao rafiki wa Sportsmail inafahamu kuwa Wenger atasaini mkataba unaompatia paundi milioni 8 kwa kila msimu.
Na atapewa bajeti kubwa zaidi katika
historia ya Asernal ili kumsaidia kushinda taji la ligi kuu msimu ujao
kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.
Mwisho wa siku Wenger alishika kombe mkononi mwake katika uwanja wa Wembley kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005
0 comments:
Post a Comment