Polisi nchini Japan wanachunguza kisa cha kushangaza
ambapo maiti ya mwanamke aliyeuawa ilitumwa kutoka Osaka hadi Tokyo kwa
njia ya posta.
Inaaminika mwanamke huyo, Rika Okada, alidungwa
kisu na mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku ambayo ilitiwa kibandiko na
karatasi iliyosema kuwa sanduku hiyo ilikuwa imemeba mwanasesere.
Sanduku hiyo, iligunduliwa ikiwa katika sehemu ya kuhifadhi vitu katika kituo cha posta.
Polisi wanasema kuwa sehemu ambako sanduku hiyo
ilipatikana imewekwa, ilikuwa imekodishwa kwa kutumia kadi ya benki ya
mwanamke huyo.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alitoweka
tangu mwishoni mwa mwezi Machi, alipotuma ujumbe wa mwisho kwenye
ukurasa wake wa Facebook kwamba alikuwa anaenda kukutana na rafiki yake
wa muda mrefu ambaye alikuwa hajamuona kwa miaka mingi.
0 comments:
Post a Comment