Friday, 23 May 2014

YANGA SC: TAWI LA TANDALE LILIFUTWA KWA MUJIBU WA KATIBA, TAARIFA ZINAZOANDIKWA NI UBABAISHAJI TU

SAM_1702 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uongozi wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji alitangaza kulifuta Tawi la Tandale kutokana na kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu, ili hali likiwa halina hadhi ya kuwa Tawi Kamili.
Kufutwa kwa Tawi la Tandale kunatokana na kutotimiza idadi ya wanachama mia moja (100)  kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC, Ibara ya 6, kipengele cha 4 “Kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi. Kiwango cha chini ya idadi ya wanachama ambao wanaweza kunda tawi kisipungue watu mia moja (100)”.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

0 comments: