Tanzania imeshika nafasi ya
pili kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 29 mwaka huu) kuilaza
Afrika Kusini mabao 2-0.
Mechi hiyo ilichezwa Uwanja
wa SSKB jijini Gaborone ambapo kwa matokeo hayo Tanzania imetwaa medali ya
fedha baada ya kushika nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika nafasi ya kwanza
na kutwaa medali ya dhahabu.
Tanzania imemaliza ikiwa na
pointi kumi ambapo ilishinda mechi tatu, sare moja na kupoteza moja mbele ya
Nigeria.
Katika mechi ya kwanza
ilitoka sare ya bao 1-1, ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland wakachapwa 3-0 na
baadaye kuwafunga Afrika Kusini 2-0. Timu ya Tanzania inayofundishwa na kocha
Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria mabao 2-0.
Wachezaji 16 waliounda
kikosi hicho cha Tanzania katika michezo hiyo inayomalizika leo (Mei 30 mwaka
huu) ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka
Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius
Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas
Chindeka.
0 comments:
Post a Comment