Wednesday, 21 May 2014

HATIMAYE WILAYA YA KILOLO YAMILIKISHA MTO KWA MWEKEZAJI


VITUUGUU_94583.jpg
Shamba la vitunguu
VITUUGUU.3_73421.jpg
Msimamizi wa shamba la vitunguu la mwekezaji, Onesmo Kihaga ambaye pia ni mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kisichotumia mashine akionyesha bomba linalosafisha maji kutoka bwawani kwenda shambani.

CHEMCHEM_6db81.jpg
Chanzo cha maji kabla yakuchepushwa.
BWAWA.jpgT_235f2.jpg
Bwawa la maji
MTO_UMEKAUKA_BAADA_YA_KUCHEPUSHWA_NA_WANANCHI_MASHAMBA_KWENYE_MTO_9db46.jpg
Mto Mlaga ukiwa umekauka baada ya mkondo wake kuchepushwa na mwekezaji.
Na Mathias Canal
Wananchi wa Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Ilole wilayani KILOLO mkoani Iringa wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kwa kubinafsisha mto wa maji na kusababisha umasikini kwa wananchi wa kijiji hicho. (FS)
Wakizungumza na MjengwaBlog kijijini hapo, wanakijiji hao wamesema kuwa uongozi wa kijiji umewasaliti wananchi kwa kubinafsisha mto ambao ndio kitega uchumi cha maendeleo ya kijiji hicho, kwani mmiliki wa mto huo amewakataza wananchi kufanya shughuli zozote katika eneo la mto huo.
Kijiji cha Kitelewasi kipo umbali wa kilomita 25 kutoka Iringa mjini ambapo ndipo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Isaya Kivike mkazi wa Iringa mjini anamiliki mto Mlaga ambao ulikuwa tegemezi kwa wanakijiji wa Kitelewasi na vijiji vya jirani kikiwemo kijiji cha Mlolo.
Mto huo umechepushwa sehemu mbili ya kwanza ikiwa ni kuelekea kwa mmiliki wa shamba la nyanya kijijini hapo BW FREDRICK MGATA ambaye ni mkazi wa kijiji hicho na amebeba tuhuma kutoka kwa wanakijiji kuhusu uanzishaji wa kuuza maeneo ya serikali akiwa kama kivuli cha umiliki wa mashamba hayo.
ISAYA KIVIKE ambaye ndiye mmiliki mkuu wa mto huo yeye amezuia maji hayo kutoka katika maporomoko ya mlima uliopo kijijini hapo kwa kujenga bwawa ambalo maji yote yaliyotakiwa kusafiri kwenda mtoni yanaingia kwenye bwawa hilo.
Bwawa hilo lina urefu wa mita 9 kwenda chini, lakini maji yaliyopo hivi sasa bwawani hapo yana ujazo wa mita 7.5, maji ambayo huelekea kwenye shamba la vitunguu ambalo lina ukubwa wa hekari 15, lakini sehemu ya shamba yenye vitunguu kwa hivi sasa ni hekari 3.5.
kijana wa makamo ambaye hakutaka kujitambulisha, yeye alitoa tuhuma kwa FREDRICK MGATA mmiliki wa shamba la nyanya ambaye amesababisha uuzaji wa maeneo kijijini hapo kwa kujifanya kama ndiye mmiliki wa mashamba hayo kitendo ambacho wanakijiji hao wamesema kuwa hayakuwa mashamba yake bali mashamba ya serikali.
STAN MGATA mwenyekiti wa kijiji jirani cha MLOLO ambaye ni mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Kitelewasi yeye amesema kuwa kero kubwa ni kuhusu eneo lililouzwa na uongozi wa kijiji hicho takribani hekari 17, huku akisema ameshindwa kutambua haki ya wananchi mahali ilipo.
Mjumbe wa halmashauri ya kijiji MIKIDADI NGONGANGE wamewahi kumtupia lawama aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kololo wakati huo Dkt. Mfutakamba ambaye alilitupa swala hilo kwa afisa ardhi wa wilaya ya Kilolo.
Aidha NGONGANGE aliitaja mito iliyopo kijijini hapo ikiwa ni pamoja na mto Kilofi, Mlaga, na mto Ng'ezi ambapo nwenyekiti alikataa kwa kutaka mto k
Kilofi ndio mto unaotoa maji mengi hivyo hakuna haja ya kutaka mto Mlaga.
Hata hivyo mwenyekiti wa kijiji cha Kitelewasi ULEDI NDENGA yeye alisema umiliki wa mto huo umefuata taratibu zote za kisheria kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya na hatimaye kupewa kibali na ofisi ya bonde la mto Rufiji (Rufiji Basin).
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ilole JOHN MPONDA amekiri kuwa ISAYA KIVIKE anamiliki mto huo lakini anamiliki kihalali kutokana na makubaliano kati yake na serikali ya kijiji japo amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ubinafsishaji wa mto huo.

0 comments: