Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA), Eliud
Mvella amejiunga na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
Amejiunga
na Sekretarieti ya TFF katika Idara ya Sheria na Vyama Wanachama
kuanzia leo (Mei 21 mwaka huu) ambapo atashughulikia masuala ya
wanachama.
Mvella
alijiuzulu rasmi wadhifa wake IRFA jana (Mei 20 mwaka huu). Mwenyekiti
wa IRFA, Cyprian Kwihyava amepokea barua ya kujiuzulu huko ambapo
ameelezea masikitiko yake kwa uamuzi huo wa Mvella.
Ni
imani ya TFF kuwa Mvella atatumia uzoefu wake wa muda mrefu katika
uongozi wa mpira wa miguu kuhakikisha TFF inaimarisha uhusiano wake na
wanachama wake.
TFF ina wanachama 44 ambao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment