WAKAZI wa
mkoa wa Lindi wametakiwa kutodanganyika na kundi la watu wachache,
wanaotaka kuvuruga amani iliyopo, bali waitunze na kuhakikisha haipotei,
kwani amani ikitoweka hao wanaowadanyanga, watakimbia na kuwaacha
wakiteseka.
Wito huo
ulitolewa na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa
Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya CCM wakati wa sherehe za Chama Cha
Mapinnduzi (CCM) kutimiza miaka 37.
Sherehe hizo zilifanyika katika kata ya Kiwalala wilaya ya Lindi Vijijini.
Mama
Kikwete alisema CCM imefanya mambo mengi katika harakati za ukombozi
Barani Afrika, kwani Tanzania ilikuwa kimbilio la wanyonge kwa kuwa
wapigania uhuru wengi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika ambazo hazikuwa
zimepata uhuru, walipokelewa , walihifadhiwa , walisaidiwa na kuwakarimu
kwa dhati, jambo ambalo si dogo na hii yote ilitokana na amani iliyopo.
“Chama
chetu kimefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuleta demokrasia ya
vyama vingi toka mwaka 1992 na leo hii tunatimiza miaka 22 ndani ya
mfumo wa vyama vingi huku tukiwa na amani, umoja na ushikamano miongoni
mwa watanzania, tumeleta usawa kwa wananchi wote bila kujali jinsia,
rangi kabila wala dini. Chama cha Mapinduzi, kupitia Serikali zake,
kinawajali wananchi kwa kuwasogezea huduma mbalimbali za kijamii hadi
vijijini na kupanua fursa za kiuchumi na kimaendeleo kwa wananchi”,
alisema Mke wa Rais.
Kwa
upande wake, Mlezi wa Chama hicho Mkoa wa Lindi, Dk. Maua Daftari
aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa na umoja na mshikamano na kwa
kufanya hivyo wataweza kushinda na kutekeleza ilani ya chama chao.
CHANZO:HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment