Monday, 3 February 2014

COPA del REY: NUSU FAINALI JUMATANO!

>>NI EL DERBI MADRILEÑO: REAL MADRID v ATLETICO MADRID!!
>>KUFUATIA BARCA v REAL SOCIEDAD!
ATLETICO-COPA_DEL_REYNUSU FAINALI za Kombe la Mfalme huko Spain, Copa del Rey, zitachezwa Jumatano Usiku ambapo Wakongwe wa huko, Real Madrid na Barcelona, zitaanza kucheza Nyumbani kwao na kurudiana Ugenini.
Hiyo Jumatano Februari 5, Mechi ya kwanza itachezwa El Estadio Santiago Bernabeu ambapo Wenyeji Real Madrid watawakaribisha Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, ambao pia ni Vinara wa La Liga, Atletico Madrid, ambao pia ni Mahasimu wao wakubwa kwenye Dabi ya Jiji la Madrid, maarufu kama El Derbi madrileño.
Baada ya Mechi hiyo itafuata Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali nyingine huko Nou Camp kati ya Barcelona na Real Sociedad.
Marudiano ya Nusu Fainali hizi ni Wiki ijayo.
COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 5
22:00 Real Madrid CF v Atletico de Madrid [El Estadio Santiago Bernabeu]
24:00 FC Barcelona v Real Sociedad [Camp Nou]
Marudiano
Jumanne Februari 11
23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19

Related Posts:

0 comments: