Sunday, 2 February 2014

VPL: YANGA YAICHAPA MBEYA CITY 1-0! NA AZAM YAINYUKA KAGERA, 4-0

>>AZAM YAINYUKA KAGERA, YABAKI KILELENI!
MATOKEO:
Jumapili Februari 2
Yanga 1 Mbeya City 0
Azam 4 Kagera Sugar 0

yangaaa 
LEO, Jijini Dar es Salaama zilichezwa Mechi mbili za VPL, Ligi Kuu Vodacom, zikihusisha Timu 3 za juu na Azam FC kubaki kileleni baada kuinyuka Kagera Sugara Bao 4-0 huko Azam Complez, Chamazi na Yanga kuipa kipigo cha kwanza kwenye Ligi Mbeya City na kubaki Nafasi ya Pili.
SOMA ZAIDI:
YANGA 1 MBEYA CITY 0
Bao la Dakika ya 16 la Supastraika, Mrisho Ngassa, liliwashushia Mbeya City kipigo cha kwanza kwenye Ligi na kuifanya Yanga izidi kujichimbia Nafasi ya Pili ikiwa Pointi 1 nyuma ya Azam FC.
Mbeya City, ambao walipigana kiume, walipata pigo mara tu baada Kipindi cha Pili kuanza baada ya Mchezaji wao Steven Mazanda kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
 
AZAMFC 4 KAGERA SUGAR 0
Huko Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salamm, Wenyeji na Vinara wa VPL, Azam FC, waliendelea kukaa kileleni baada kuinyuka Kager Sugar Bao 4-0.
Bao za Azam FC zilifungwa na Brian Umony, Bao mbili, na nyingine kupitia Jabir Aziz Stima na Kevin Friday.
 
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano  Februari 5
Tanzania Prisons vs Coastal Union 
(Uwanja wa Sokoine, Mbeya)

Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting 
(Uwanja wa Mkwakwani, Tanga)

Rhino Rangers vs Oljoro JKT 
(Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora)

JKT Ruvu vs Ashanti United 
(Uwanja wa Azam Complex, Chamazi)
MSIMAMO:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
29
10
19
36
2
Young Africans
16
10
5
1
34
12
22
35
3
Mbeya City
16
8
7
1
22
13
9
31
4
Simba SC
15
8
6
1
31
13
18
30
5
Mtibwa Sugar
15
5
6
4
19
18
1
21
6
Kagera Sugar
16
5
6
5
15
15
0
21
7
Coastal Union
15
3
9
3
11
8
3
18
8
Ruvu Shootings
14
4
6
4
16
16
0
18
9
JKT Ruvu
14
6
0
8
13
18
-5
18
10
Rhino Rangers
15
2
5
8
9
18
-9
11
11
JKT Oljoro
15
2
5
8
10
15
-5
11
12
Ashanti United
15
2
4
9
13
28
-15
10
13
Tanzania Prisons
13
1
6
6
6
16
-10
9
14
Mgambo JKT
15
2
3
10
7
26
-19
9

TAARIFA TOKA TFF:
Release No. 016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 2, 2014
TARIMBA KUONGOZA KAMATI YA NIDHAMU
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa wajumbe kuunda kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili za rufani za vyombo hivyo.
Rais wa zamani wa Yanga, Tarimba Abbas ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza Kamati ya Nidhamu. Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
TFF, CRDB KUTATHIMINI TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeagiza kifanyike kikao cha dharura kati ya Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za elektroniki.
Lengo la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.
Viwanja vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.
MECHI YA STAND, KANEMBWA MEZANI TENA
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini Shinyanga.
Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.
Pia Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Related Posts:

0 comments: