Naibu Waziri, Amos Makalla akiwa katika mradi wa maji, kijiji cha Lupiro.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla amemaliza ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Mhe.
Makalla amemaliza ziara hiyo kwa kutembelea miradi ya maji ya
Halmashauri za Wilaya za Ulanga na Kilombero na kukagua utekelezaji
wake.
“Utekelezaji
unaenda vizuri, isipokuwa kasi iongezwe ili miradi yote ikamilike kwa
wakati, na nitafuatilia kwa ukaribu miradi yote niliyoikagua na nitarudi
kuangalia maendeleo yake”. Wakati umefika kuhakikisha sekta ya maji
inatekeleza sera zake ipasavyo na kuachana na masuala ya siasa kama
wananchi walivyozoea na kusababisha kukosa imani na Serikali yao”,
alisema Mhe. Makalla.
Naibu
Waziri aliendelea kwa kusema Serikali imetenga pesa za kutosha
kukamilisha miradi hii, kwa hiyo, hakuna sababu nyingine yoyote ya
kutokamilisha miradi hii. Nataka nisikie wakandarasi wamekamilisha
miradi hii na wanadai pesa za malipo na sio wanadai wakati kazi
hazifanyiki. Ninachosisitiza ni ufuatiliaji wa karibu kwa watendaji wote
wa Serikali na kuhakikisha kazi inafanyika vizuri bila visingizio
vyovyote.
“Nimeahidiwa
kuwa mradi wa kijiji cha Lupiro utakuwa umekamilika ifikapo tarehe
01/03/2014. Hivyo, nategemea kuja kuufungua rasmi siku hiyo ili wakazi
wa hapa na jirani zake waanze kupata maji safi na salama”, aliongeza
Naibu Waziri Makalla.
Aidha,
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mji wa
Morogoro (MORUWASA), Inj. Halima Mbiru alisema Serikali, Halmashauri na
MORUWASA kila mmoja imetenga fedha za kutosha katika kutekeleza miradi
yake yote kwa muda uliopangwa. Akasisitiza kujituma na kufanya bidii kwa
wahusika wote ili kufanikisha lengo hilo na kuondokana na tatizo la
maji mkoani humo.
Mhe.
Makalla alitembelea kijiji cha Lupiro ambacho ni moja ya vijiji kumi,
vinavyotekeleza mpango wa BRN. Pia, alifika kwenye chanzo cha maji cha
Kibulubutu, wilayani Kilombero ambacho Serikali ina mpango kutumia maji
yake kwa wakazi wa mji huo katika azma ya kumaliza tatizo la maji.
Hii
ni ziara ya pili ya Naibu Waziri, Amos Makalla tangu aanze kazi katika
Wizara ya Maji baada ya ile ya kwanza aliyoanza Dar es Salaam wiki tatu
zilizopita.
Kituo cha kusukumia maji na tanki la kuhifadhi maji katika mradi wa maji, kijiji cha Lupiro
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, (kushoto) pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Serikali katika mradi wa maji wa Ulanga mjini.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akipokea zawadi ya kifaa cha kuchujia maji kwa ajili ya kupata maji safi na salama ya kunywa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MSABI ya wilaya ya Kilombero, Dale Young.
0 comments:
Post a Comment