UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, imerudi kwa makeke kwa Timu za Nyumbani zote kutandikwa wakati Barcelona
walipoiwasha
Manchester City 2-0 huko Etihad na Paris Saint-Germain kuitandika Bayer
Leverkusen Bao 4-0 huko Bay Arena, Jijini Leverkusen, Ujerumani, hizo
zikiwa Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MATOKEO:
Jumanne Februari 18
Manchester City 0 FC Barcelona 2
Bayer 04 Leverkusen 0 Paris Saint-Germain 4
MANCHESTER CITY 0 BARCELONA 2
PENATI ya Dakika ya 54 ya Lionel Messi
iliwafungulia njia Barcelona na kupata ushindi wa Bao 2-0 walipocheza na
Manchester City Uwanjani Etihad katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Penati hiyo ilitolewa baada ya
Demichelis kumwangusha Messi aliekuwa anaenda kukutana na Kipa Joe Hart
na pia kusababisha Beki huyo wa Man City kupewa Kadi Nyekundu na Refa
Jonas Eriksson kutoka Sweden.
DONDOO MUHIMU:
-BARCA hawana mawindo mema Jiji la MANCHESTER:
-JIJINI MANCHESTER, BARCA wamecheza Mechi 4 Old Trafford na hawakushinda hata moja kwa Kufungwa 2, Sare 2 dhidi ya MAN UNITED!
-Wamecheza na Man City Mechi 6 za Kirafiki na Kushinda 3, Kufungwa 3 moja ikiwa ni ya Ufunguzi wa City
of Manchester Stadium Tarehe 10 Agosti 2003 na City kushinda Bao 2-1
kwa Bao za Nicolas Anelka na Trevor Sinclair na la Barca kufungwa na
Javier Saviola.
Barcelona walifunga Bao lao la Pili
katika Dakika ya 90 kupitia Dani Alves baada ya kazi nzuri ya Neymar
alieingia Kipindi cha Pili.
Timu hizi zitarudiana huko Nou Camp hapo Machi 12 na City watahitaji kushinda Bao 3-0 ili wasonge Robo Fainali.
VIKOSI:
MANCHESTER CITY [Mfumo 4-5-1]: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Jesús Navas, Silva, Fernandinho, Y. Touré, Kolarov, Negredo
Akiba: Pantilimon, Richards, Lescott, Nasri, Javi García, Džeko, Jovetić.
BARCELONA [Mfumo 4-3-3]: Víctor Valdés, Piqué, Mascherano, Jordi Alba, Daniel Alves, Fàbregas, Xavi Hernández, Iniesta, Busquets, Alexis Sánchez, Messi
Akiba: Pinto, Bartra, Adriano, Song, Sergi Roberto, Pedro Rodríguez, Neymar.
REFA: Jonas Eriksson [Sweden]
BAYER LEVERKUSEN 0 PARIS SAINT-GERMAIN 4
Wakicheza kwao BayArena Jijini Lerkusen,
Nchini Germany, Bayer Leverkusen wametandikwa Bao 4-0 na Paris
Saint-Germain ambao hadi Mapumziko walikuwa mbele kwa Bao 3-0.
Bao za PSG zilifungwa na Blaise Matuidi,
Dakika ya 3, na mbili za Zlatan Ibrahimovic, kwenye Dakika ya 39 kwa
Penati na jingine kwa mzinga mkali nje ya Boksi katika Dakika ya 42 huku
Bao la 4 likipachikwa na Yohan Cabaye kwenye Dakika ya 88.
Kuanzia Dakika ya 59, Leverkusen walicheza Mtu 10 baada ya Emir Spahic kupewa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano mbili.
VIKOSI:
Leverkusen: Leno, Hilbert, Spahic, Toprak, Guardado, Bender, Rolfes, Castro, Sam, Kiessling, Son
Akiba: Yelldell, Reinartz, Wollscheid, Hegeler, Oztunali, Boenisch, Brandt.
PSG: Sirigu, van der Wiel, Alex, Thiago Silva, Maxwell, Verratti, Motta, Matuidi, L. Moura, Ibrahimovic, Lavezzi
Akiba: Douchez, Pastore, Cabaye, Marquinhos, Menez, Digne, Rabiot.
REFA: Viktor Kassai (Hungary)
UEFA CHAMPIONZ LIG
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP
0 comments:
Post a Comment