Tuesday, 18 February 2014

UCL: LEO JUMATANO NI AC MILAN v ATLETICO MADRID NA ARSENAL v BAYERN MUNICH

   

>>NI BALOTELLI v DIEGO COSTA!!
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich

AC_MILAN_v_ATLETICOSTRAIKA hatari wa Atletico Madrid Diego Costa, Mzawa wa Brazil alieikanaBALOTELLINchi yake na kuamua kuichezea Spain, amewaonya wenzake kuwa watakuwa na balaa kubwa Jumatano Usiku ndani ya Stadio Guiseppe Meazza, maarufu kama San Siro, ikiwa watapuuza tishio la ‘Mwana Mtukutu’ Mario Balotelli wa AC Milan katika Mechi yao ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Atletico, ambao wako juu wakifungana kwa Pointi na Vigogo Barcelona na Real Madrid kwenye La Liga huko Spain, wanakutana na AC Milan ambayo inasuasua kwenye Serie A ikiwa Nafasi ya 9 na wako Pointi 31 nyuma ya Vinara Juventus.
Lakini Diego Costa ameonya kuwa itakuwa ujinga mkubwa kuidharau AC Milan ambayo imetwaa Ubingwa wa Ulaya mara 7.
DIEGO_COSTADiego Costa amenena: “Itakuwa Mechi ngumu ndani ya San Siro lakini nzuri. Milan wana utamaduni mzuri kwenye Mashindano haya na wanajua namna ya kucheza Gemu kama hizi. Inabidi tufanye kazi.”
Pia Costa ameonya kuhusu hatari ya Mario Balotelli na kuwataka Mabeki wake kuwa makini.
Kwa Atletico Madrid, ambao wako chini ya Meneja Diego Simeone, hii ni mara ya kwanza kwao kufika Hatua ya Mtoano ya UCL tangu Mwaka 2008/09 na hawajavuka zaidi ya Robo Fainali tangu 1997.
Hivi sasa AC Milan ipo chini ya Kiungo wao wa zamani Clarence Seedorf ambae amechukua wadhifa wa Meneja Mwezi uliopita baada ya kutimuliwa Massimiliano Allegri.
Seedorf ashawahi kutwaa Ubingwa wa Ulaya mara 4 akiwa kama Mchezaji lakini ana kibarua kigumu kwani Timu yake ina upungufu mkubwa wa kuwakosa Viungo Sulley Muntari na Riccardo Montolivo, ambao wako Kifungoni, na Majeruhi Stephan El Shaarawy na Robinho wakiwa ni miongoni mwa Wachezaji 6 ambao wana maumivu.

  UCL: JUMATANO NI ARSENAL v BAYERN MUNICH

UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich

KWA wale Wadau wa Arsenal wanajua fika kuwa katika Miaka ya hivi karibuni Mwezi Februari ndio huwavunja mioyo na Jumatano Usiku wana kibarua kigumu kwa kuikaribisha Emirates Bayern Munich, Mabingwa wa Ulaya, katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mwaka Jana, Arsenal walifungwa kwao Emirates na Blackburn Rovers na kutupwa nje ya FA CUP na Siku chache baadae kutandikwa Bao 3-1 na Bayern Munich katika Mechi kama hii ya UCL na kuumaliza kabisa Msimu wao huo lakini Msimu huu Juzi wameipiga Liverpool Bao 2-1 na kuitupa nje ya FA CUP na hii ni ishara njema kwao.

Uso kwa Uso:
USHINDI: Bayern Mechi 3 Arsenal Mechi 2

PEP_v_WENGERLakini Bayern Munich ni moto mwingine na Arsenal itatinga kwenye Mechi hii ikiwa na mapengo kwa kuwakosa Majeruhi Aaron Ramsey na Theo Walcott na pia Mikel Arteta ambae yuko Kifungoni.
Lakini badala yake wanaweza kuwatumia Alex Oxlade-Chamberlain na Tomas Rosicky huku katikati kwenye Kiungo wakisimama Mathieu Flamini na Jack Wilshere.
Nae Pep Guardiola, Meneja wa Bayern Munich, ana pigo kubwa la kumkosa Mchezaji alieingia Fainali ya Ballon d'Or, Franck Ribery, ambae Juzi alifanyiwa operesheni ndogo ya kutibu Mshipa wa Damu uliokuwa ukivuja kwenye Makalio yake.
Kawaida mrithi wa Ribery angekuwa Winga wa Uswisi, Xherdan Shaqiri, lakini nae ana matatizo ya Musuli.
Bayern wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na Rekodi nzuri ya kushinda Mechi zao 9 zilizopita na kufunga Jumla ya Bao 28 na kufungwa 2 tu.

UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 18
22:45 Manchester City v FC Barcelona
22:45 Bayer 04 Leverkusen v Paris Saint-Germain
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP

Related Posts:

0 comments: