……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Muheza
Mashindano
ya ngalawa yaliyofanyika jana Wilayani Muheza katika Kijiji cha Kigombe
yamefana huku Kampuni ya simu ya ZANTEL ikifanikisha kwa kutoa zawadi .
Kutokana
na hali hiyo Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika mashindano hayo amewataka vijana washiriki katika
michezo badala ya kukaa vijiweni.
Kauli
hiyo aliitoja wakati akifungua mashindano ya kwanza ya Ngalawa mkoani
Tanga yaliyofanyika kwenye Pwani ya Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza.
Mwidau
alisema kupitia michezo vijana wataweza kupata fursa nyingi ikiwemo
elimu na ujunzi kutoka kwa wenzao ,burudani pamoja na kujenga afya za
kimwili na kiakili.
“Mahindano
haya ya Ngalawa hapo awali yalikuwa yanafanyika ngazi ya kijiji lakini
kupitia kwa wadhamini Kampuni ya simu ya ZANTEL tumeweza kuyafanya
kimkoa kwa lengo la kuibua fursa za ajira kwa vijana na kwashirikisha
watu katika michezo, ”alisema Mwidau.
Nae
Meneja mauzo wa ZANTELTanzania Salum Ngururu, alisema kuwa lengo la
kudhamini mashindano hayo ni kurudisha faida wanayopata kwa jamii
kutoka na huduma zake na kuendelea kuwatambulisha bidhaa zinazotolewa na
kampuni hiyo.
Alisema ZANTEL itakuwa ikiboresha zawadi za mashindano hayo kila mwaka ili yaweze kuvuta washiriki wengi.
Mshindi wa kwanza alijipatia kitita cha Shilingi laki tatu, kikombe cha ushindi pamoja na medali za dhahabu.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka ambaye aliweza kujinyakuliwa zawadi hiyo.
Mashindano
hayo yalishirikisha jumla ya Ngalawa thelathini zilizokuwa na washiriki
watano ambapo washiriki walitoka katika Wilaya za Tanga, Pangani na
Muheza huku Wilaya ya Mkinga ikishindwa kushiriki kutokana na kushindwa
kufanya maandalizi mazuri.
0 comments:
Post a Comment