Chama
Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Singida mjini jana kimefanya matembezi ya
mshikamano ya kilometa kumi kuanzsia ofisi ya CCM mkoa wa Singida hadi
Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida.
Baadhi
ya wanachama wa CCM manispaa ya Singida,wakishiriki matembezi ya
mshikamano ya kilomita kumi ikiwa ni sehemu ya sherehe ya maadhimisho ya
CCM kutimiza miaka 37 toka kianzishwe.(Picha na Nathaniel Limu).
Katibu
wa CCM mkoa wa Singida,Naomi Kampambala ( mstari wa pili wa kwanza
kulia mwenye kofia kapelo) akijumuika na wanaCCM wa manispaa ya
Singida,kwenye matembezi ya mshikamano yaliyofanyika jana ya kilomita
kumi.
Mstahiki
meya wa halmashauri ya manispaa ya Singida na sheikh wa mkoa wa
Singida,Sheikh Salum Mahami,(wa pili kushoto) akishiriki matembezi ya
kilomita kumi ya mshikamano ya CCM yaliyofanyika jana 02/02/2014. Wa
kwanza kushoto ni katibu wa wazazi CCM mkoa wa Singida,Bwiga na watatu
kushoto ni mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM taifa manispaa ya
Singida.Hassan Mazala.
0 comments:
Post a Comment