Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wakazi
wa mkoa wa Lindi wametakiwa kutodanganyika na kundi la watu wachache
wanaotaka kuvuruga amani iliyopo bali waitunze na kuhakikisha kuwa
haipotei kwani amani ikitoweka hao wanaowadanyanga watakimbia na
kuwaacha wakiteseka .
Wito
huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa wakati wa uzinduzi wa sherehe za
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinnduzi (CCM) mkoani Lindi zilizofanyika
katika kata ya Kiwalala wilaya ya Lindi vijijini ambapo chama hicho
kinatimiza miaka 37.
Mama
Kikwete alisema CCM imefanya mambo mengi katika harakati za ukombozi
Barani Afrika kwani Tanzania ilikuwa kimbilio la wanyonge kwa kuwa
wapigania uhuru wengi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika ambazo hazikuwa
zimepata uhuru walipokelewa , walihifadhiwa , walisaidiwa na kuwakarimu
kwa dhati jambo ambalo si dogo na hii yote ilitokana na amani iliyopo.
“Chama
chetu kimefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuleta Demokrasia ya
vyama vingi toka mwaka 1992 na leo hii tunatimiza miaka 22 ndani ya
mfumo wa vyama vingi huku tukiwa na amani, umoja na ushikamano miongoni
mwa watanzania, tumeleta usawa kwa wananchi wote bila kujali jinsia,
rangi kabila wala dini.
Chama
cha Mapinduzi kupitia Serikali zake zinawajali wananchi kwa kuwasogezea
huduma mbalimbali za kijamii hadi vijijini na kupanua fursa za
kiuchumi na kimaendeleo kwa wananchi”, alisema Mke wa Rais.
Aidha
Mjumbe huyo wa NEC pia aliwataka wananchi hao kujishughulisha na kazi
mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kulima japo mazao ya
chakula kama muhogo kwani Serikali tayari imeshafanyia mambo mengi ya
maana ambayo yanawasaidia katika shughuli zao za maendeleo.
Mama
Kikwete alisema, “Serikali imejenga Shule, Hospitali, barabara na
kuimarisha miundombinu ya barabara na leo hii kama mtalima kwa bidii
mtaweza kusafirisha na kuuza mazao yenu mbali na hapa kwakuwa barabara
ni nzuri na usafiri ni wa uhakika”.
Kwa upande wake Mlezi wa Chama hicho katika mkoa
wa Lindi Dk. Maua Daftari aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa na
umoja na mshikamano kwa kufanya hivyo wataweza kushinda na kutekeleza
ilani ya chama chao.
Katika
uzinduzi wa sherehe hizo ambazo kilele chake kitafanyika kesho katika
wilaya ya Ruangwa jumla ya wanachama 17 walijiunga na chama hicho
ambapo wanachama wapya ni 12, kutoka chama cha upinzani cha Civic United Front(CUF) wanne na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mmoja.
0 comments:
Post a Comment