TARIMBA KUONGOZA KAMATI YA NIDHAMU
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya
uteuzi wa wajumbe kuunda kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili
za rufani za vyombo hivyo.
Rais wa zamani wa Yanga, TarimbaAbbas
ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza Kamati ya Nidhamu.
Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu
Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati
ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo
wakati makamu wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa
kamati hiyo ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza
Kamati ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria
Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani
Lindi, Said Mtanda.
Kamati
ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema
(Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari,
Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
TFF, CRDB KUTATHIMINI TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeagiza
kifanyike kikao cha dharura kati ya Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi
Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya
matumizi ya tiketi za elektroniki.
Lengo
la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa
tiketi za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.
Viwanja
vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja
hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na
CCM Kirumba.
MECHI YA STAND, KANEMBWA MEZANI TENA
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza
mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo
hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1
mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo
iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini Shinyanga.
Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.
Pia
Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio
hilo la Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT
waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment