Saturday, 1 February 2014

MAJANGA YANAENDELEA MAN UNITED, YAPIGWA NA STOKE CITY 2-1

>>EVERTON YASHINDA, SPURS YABANWA!

>>JUMAPILI: ARSENAL v PALACE, WBA v LIVERPOOL!
MATOKEO:
Jumamosi Februari 1
Newcastle 0 Sunderland 3
West Ham 2 Swansea 0
Cardiff 2 Norwich 1
Everton 2 Aston Villa 1
Fulham 0 Southampton 3
Hull 1 Tottenham 1
Stoke 2 Man Utd 1

STOKE CITY 2 MAN UNITED 1
 
Bao mbili za Charlie Adam zimewapa Stoke ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi tangu Mwaka 1984 dhidi ya Man United walipoichapa 2-1 Uwanjani Britannica.
Man United, wakianza Mechi kwa kuwachezesha kwa pamoja kwa mara ya kwanza Juan Mata, Robin van Persie na Wayne Rooney, walipata pigo kwa kuwapoteza Msentahafu wao wawili Jony Evans na Phil Jones walioumia Kipindi cha Kwanza tu, na bahati ilizidi kuwa mbaya kwao baada ya Frikiki ya Adams kumbabatiza Michael Carrick na kutinga wavuni.
Baada Kipindi cha Pili kuanza, Van Persie aliisawazishia Man United lakini Shuti la Mita 25 la Adams liliwapa ushindi Stoke.
 

CARDIFF CITY 2 NORWICH CITY 1
Cardiff walitoka nyuma na kuichapa Norwich Bao 2-1 na kujinasua toka mkiani na kumpa Pointi za kwanza Meneja Ole Gunnar Solskjaer.
Robert Snodgrass aliipa Norwich Bao la kuongoza lakini Mchezaji mpya wa Mkopo kutoka Man United, Wilfried Zaha, alitoa pasi safi kwa Craig Bellamy na kisha mpya mwingine, Kenwyne Jones, kuwapa ushindi kwa kufunga Bao la Pili.
 
EVERTON 2 ASTON VILLA 1
Everton walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuifunga Villa Bao 2-1 kwa Bao za Naismith na Mirallas na Bao la Villa kufungwa na Bacuna.
 

FULHAM 0 SOUTHAMPTON 3
Bao 3 za Kipindi cha Pili za Lallana, Lambert na Rodriguez, zimewapa ushindi Southampton wa Bao 3-0 walipoichapa Fulham iliyokuwa kwao Craven Cottage na kuitupa mkiani mwa Ligi.
 
HULL CITY 1 TOTTENHAM 1
Hull na Tottenham zilitoka Sare ya Bao 1-1 baada ya Paulinho kuisawazishia Tottenham Bao wakati Hull walipotangulia kwa Bao la Long.
 
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 2
16:30 West Brom v Liverpool
19:00 Arsenal v Crystal Palace
Jumatatu Februari 3
23:00 Man City v Chelsea
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Man City 23 42 53
2 Arsenal 23 24 52
3 Chelsea 23 23 50
4 Liverpool 23 29 46
5 Everton 24 12 45
6 Tottenham 24 -1 44
7 Man Utd 24 10 40
8 Newcastle 24 1 37
9 Southampton 24 7 35
10 Aston Villa 24 -7 27
11 Stoke 24 -14 25
12 Swansea 24 -6 24
13 Hull 24 -7 24
14 Sunderland 24 -11 24
15 Norwich 24 -18 24
16 Crystal Palace 23 -16 23
17 West Brom 23 -6 22
18 West Ham 24 -9 22
19 Cardiff 24 -22 21
20 Fulham 24 -31 19

0 comments: