Saturday, 1 February 2014

HII NI RASIMI WAYNE ROONEY SASA KUBAKI MAN UNITED

rooney1 337d8

 

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney amekubali kusaini mkataba mpya utakaomweka Old Trafford zaidi ya mwaka 2015 huku akiwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo. 
Rooney amesuasua kusaini mkataba mpya Old Trafford na ilidaiwa kwamba alikuwa anajiandaa kuondoka mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kupata changamoto mpya ya soka nje ya Man United.
Mkataba wa Rooney unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao Juni 2015 na kulikuwa na wasiwasi kwamba staa huyo wa zamani wa Everton alikuwa anataka kuondoka bure mwishoni mwa msimu ujao hili apate fedha nyingi zaidi.
Hata hivyo, kocha David Moyes amefanikiwa kumshawishi nyota huyo kubaki lakini kwa gharama za kumlipa mshahara wa Pauni 300,000 (Sh.750 milioni) kwa wiki ambao unaweza kuwa wa mwisho kwake klabuni hapo.
Wakati huohuo, licha kumnasa kiungo mchezeshaji wa Chelsea, Juan Mata na kufanikiwa kumbakiza Rooney, Moyes amekumbana na pigo baada ya kiungo wa Juventus aliyekuwa anamwinda, Arturo Vidal kusisitiza kwamba atabaki klabuni hapo.
Moyes ameshasafiri mpaka Italia kwa ajili ya kumwangalia nyota huyo wa kimataifa wa Chile ambaye yupo katika kiwango cha juu na alikuwa anataka kumchukua katika kikosi chake kwa ajili ya kukitia makali na kukirudisha katika ushindani.
Moyes atalazimika kuongeza juhudi zake kwa kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos ambaye anaweza kuuzwa. Chanzo: mwanaspoti

0 comments: