………………………………………………………………
NA MA GRETH KINABO- MAELEZO
Mwenyekiti wa
muda wa Bunge Maalum la Katiba, Ameir Pandu Kificho, ametangaza tume ya
sita kwa ajili ya kujadili kuhusu malalamiko ya posho ya Sh. 300,000
yaliyotolewa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum ya Katiba kuwa
haitoshi kuweza kuifanya kazi hiyo kwa umakini.
Kificho
alitangaza majina hayo jana mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa semina kwa
wajumbe hao leo mjini Dodoma kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Bunge la
Katiba Sura ya 83 toleo la mwaka 2014.
“Kuhusu suala la kumudu kuishi vizuri na hii kazi nzito tuliyonayo bado halina majibu kwa sasa ,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aliyataja
majina hayo kuwa ni William Lukuvi, Mohammed Aboud Mohammed, Freeman
Mbowe ,Paul Kimiti , Asha Bakari Makame na Jenista Mhagama.
Alisema timu
hiyo itakutana mara baada ya semina hiyo leo na ikiongozwa na
Mwenyekiti huyo wa muda ili kuweza kukaa pamoja na kupanga ya kuweza
kuiomba Serikali kuangalia jambo hilo na kuweza kupata majibu.
Timu hiyo imeundwa baada ya baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kulalamikia posho hizo ndani na nje ya ukumbi wa Bunge jana.
0 comments:
Post a Comment