Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu (UNFPA), Bibi Mariam Khan leo alitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na kutoa wito kwa serikali kufanya hima katika kukabiliana na changamoto za ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa mijini nchini Tanzania.
Hata
hivyo, Bibi Khan alisema kuwa licha ya kuwa ongezeko la idadi ya watu
linaathari mbalimbali kama lisipothibiwa, Tanzania inaweza kutuma fursa
hiyo kwa kuwekeza kwa vijana kama nguvu kazi kwa shughuli za kimaendeleo
ili kuongeza pato na uchumi wa taifa.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa serikali inatambua changamoto
hizo, na kuwa kwa sasa inajipanga kuipitia Sera ya Idadi ya Watu ya
Mwaka 2006 ili iendane na changamoto hizo.
Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia)
akiangalia takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini
Tanzania. Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam
Khan (Wa pili kulia) aliyembelea Ofisi za Tume ya Mipango leo. Wengine
pichani ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya
Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Mchambuzi Mkuu wa Sera, Bw.
Edwin Ninde (Wa pili kushoto) na Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu
toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu. 
Naibu
Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi
Florence Mwanri (Kushoto) akifuatilia kwa makini takwimu zinazohusiana
na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania zilizokuwa zikiwasilishwa na
Bibi Mariam Khan (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Tume ya
Mipango. Kulia ni Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango), Bw. Edwin Ninde. 
0 comments:
Post a Comment