Wednesday, 24 September 2014

NYUMB YAWAKA MOTO YAUA WAWILI MKOANI IRINGA

Watu wawili wamefariki mkoani Iringa katika matukio mawili tofauti likiwepo la watoto wawili kufariki kwa kuungua moto baada ya nyumba yao kuwaka moto.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kamanda wa jeshi ala polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema nyumba ya Regani kivembela umri miaka 26 iliwaka moto na kupelekea vifo vya watoto wake wawili ambao ni Regani kivembela umri miaka 5 mwanafunzi wa chekechea ya Lukani na daeus Kivembela umri miaka 2.5
Kamanda Mungi ameongeza kuwa chanzo cha moto huo ni kutokana na mama mzazi wa watoto hao kusahau sufuria jikoni aliyoinjika njegere na kwenda kwa jilani zake ambapo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo. 

0 comments: