Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), na Katikati ni msanii nguli wa kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto.(Picha na Maktaba).
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
Mfuko wa Pensheni (PSPF) umedhamini siku ya Msanii Tanazania itayoadhimishwa Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City kwa dhumuni la kuwapa mafunzo wasanii ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi amesema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Sanaa ni kazi” ambayo itajumisha fani mbalimbali kama vile Taarabu, Muziki wa dansi, ngoma za asili na muziki wa msanii kutoka nje ya nchi.
Njaidi ameongeza kuwa fani nyingine ni uchezaji shoo, dansi za mitaani, Bongo fleva, maonesho ya mitindo ya mavazi, sanaa kwa watoto na maonesho ya sanaa ya ufundi.
“Tumeona umuhimu wa kuwepo kwa maadhimisho haya kama vile Mei Mosi, siku ya UKIMWI Duniani, Siku ya Wanawake Duniani ikiwa ni chachu ya kuhamasisha wasanii na wadau wake kuthamini sanaa nchini” alisema Njaidi.
Siku ya Msanii ni mradi uliobuniwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na kampuni ya Haak Neel Production ili kuungana na wa sanii dunia ni kote kuadhimisha siku ya kimataifa ya Msanii inayofanyika kila mwaka kwa lengo la kumtambua msanii, kazi zake na mchango wake katika jamii.
Aidha,Njaidi alisema kuwa PSPF imekuwa mstari wa mbele kutoa fursa kwa watu wote kujiunga na mfuko kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni.
Zaidi ya hayo Njaidi amesema kuwa wasanii wamejiajiri na hawana mpango mzuri wa kuweka akiba ya uzeeni, huvyo PSPF imeamua kushirikiana na BASATA katika kuandaa Siku ya Msanii kwa kuwapa elimu wasanii wote ili waweze kujiandaa kwa maisha ya badae.
Mbali na hayo PSPF inatoa fursa kwa watu wote kujiunga na mfuko kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni, hivyo kushirikiana na wasanii katika kuwapa elimu na waweze kujiandaa kwa maisha ya baadae.
0 comments:
Post a Comment