Ofisa wa Upelelezi wa Ilala, Daivd Mnyambunga katikatia akijadiliana jambo na viongozi wa CCM akiwaambia kuwa inatakiwa waondoke
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Ernest Charles akiwasihi wafuasi wake wa CCM kuondoka
Polis wakiwa wanajiandaa kwa kazi
Hapo Cuf walianzisha muzikii wakitaka kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao za mkutano
Huyu jamaa alianza kujiandaa kwa mapambano akikunja suruali
Mkuu wa upelelezi wa Ilala akaamua kumwambia aliekuwa akichezesha nyimbo wa CCM kuzima muziki haraka sana
Polis wakaendeleza doria
ASKARI Polis wa kituo cha Buguruni jana walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliokuwa wakifanya mkutano katika eneo la Buguruni Chama.
Hatua hiyo ilitokana na wanachama hao kukusanyika bila ya kuwa na vibali stahiki vya kuwawezesha kufanya mkutano wao huo ambao uliingiliana na mkutano wa Chama cha Wananchi, CUF ambao nao walikuwa wakifanyia mkutano eneo hilohilo.
Kutokana na mkanganyiko huo ambao awali ulisababisha kukunjana mashati kwa wanachama wa vyama hivyo viwili kabla ya Polis kuwasili na kutuliza vurugu hizo.
Ilichukua takribani saa tatu jeshi la Polis likiongozwa na Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolis wa Ilala, David Mnyambuga wakijadiliana na viongozi wa upande wa CUF uliokuwa ukiongozwa na Mkuu wa Habari na Uenezi wa Taifa wa chama hicho, Abdul Kambaya wakati kwa upande wa CCM ukiongozwa na Katibu wake wa Wilaya ya Ilala Ernest Charles.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea magari mawili ya Cuf yaliwasili ambapo moja liliziba magari ya Polis kwa mbele huku jingine likiwa limebeba spika za kuhutubia.
Lile lililokuwa limebeba spika liliwasha muziki wakati mazungumzo ya viongozi wa CUF, CCM pamoja na Polis yakiwa yanaendelea hali amabyo ilizua tafrani kwa kuwa wananchi wa CUF walianza kucheza na hali ambayo ilipelekea CCM nao kuwasha muziki.
Hali hiyo ilipelekea tafrani kabla ya Polisi kuzuia taaharuki hiyo na wakaendelea tena na mazungumzo, baadae iliamliwa kuwa wote wasitishe mkutano huo na kuondoka.
Kambaya akizungumza na gazeti hili alisema kuwa wamepewa vibali vyote kuanzia ofisi ya Mtendaji wa kata ya Buguruni hadi Polisi na hawawezi kusitisha mkutano huo.
Katibu wa CCM Ilala, Charles alisikika akiwataka wanachama wake kukubaliana na hoja ya Polis kuwataka kuondoka kwa kuwa hata CUF wameambiwa hivyo lakini wanachama hao walikataa kutii amri na hivyo katibu huyo alipanda gari lake na kuondoka.
Ilichukua takribani nusu kisha CUF waliwasha tena muziki uliowahamasisha wanachama wake kucheza na kisha Kambaya akaanza kuhutubia wanachana wake huku akilaani kitendo cha CCM kuingilia mkutano huo, wakati hayo yakiendelea wanachama wa CUF walianza kusogelea spika za muziki wa CCM ambao nao waliwasha tena muziki wao kwa sauti ya juu.
Kutokana na dalili hizo za kuvunjika kwa amani, Polis waliamua kuvamia eneo la CCM na kuamrisha kuzimwa kwa muziki huo na kisha kuwatawanya wanachama hao kwa mabomu ya machozi sita yaliyopigwa hewani.
Hali hiyo ilipelekea taharuki kubwa katika eneo la Buguruni huku wananchi wakikimbia hovyo huku wale waliokuwa kwenye daladala wengine kulazimika kushuka.
Baada ya takribani dakika 30 za tafrani Polisi waliendelea kuulinda mkutano wa CUF ambapo Kambaya aliendelea na kampeni ya chama chake hicho iliyokuwa ikihamasisha suala zima la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura.
0 comments:
Post a Comment