Monday, 29 September 2014

DIDIER KAVUMBAGU KUTAMBA KUHUSU UFUNGAJI BORA LIGI KUU YA TANZANZNIA BARA

 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu, ametamba kuwa sasa atahakikisha anafunga kila mechi ili kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi na hatimaye kutwaa ubingwa.

Kavumbagu ameianza Ligi Kuu Bara kwa mkwara baada ya kufunga mabao manne katika michezo miwili ya awali. Kila mchezo akitupia mawilimawili.

Akizungumza na Championi Jumatatu baada ya kuifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting juzi kwenye Uwanja wa Chamazi, Kavumbagu alisema anafurahi kuona amekuwa katika wakati mzuri ndani ya kikosi hicho lakini akasisitiza kuwa ataendelea kufunga kila anapopata nafasi.


“Cha msingi ni kufunga tu, hilo ndilo suala pekee linaloipa timu mafanikio, kwa hiyo nitajitahidi kufunga katika kila mechi kadiri ninavyopata nafasi ili kuhakikisha naisaidia timu katika mbio za kutwaa ubingwa, kisha hayo mambo ya ufungaji bora yatakuwa baadaye,” alisema Kavumbagu, mchezaji wa zamani wa Yanga.

0 comments: