Kwenye Mechi hiyo ya La Liga ambayo Barcelona waliifunga Bilbao 2-0, Kocha Luis Enrique aliwapanga Masentahafu Javier Mascherano na Jeremy Mathieu na Pique kupigwa Benchi ingawa aliingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Mascherano.
Pique amekanusha kama ana bifu na Enrique na kudai ni uamuzi wa Kocha kubadili Kikosi chake.
Hata hivyo Pique amesisitiza yeye yuko fiti na yuko tayari kucheza wakati wowote Kocha akimchagua.
Lakini hadi Leo hamna fununu yeyote kama Kocha Enrique atampanga Pique kwenye Mechi hiyo ya UCL ambayo Barca wako Kundi F pamoja na hao APOEL, Ajax na Paris St-Germain.
0 comments:
Post a Comment