KIUNGO wa Manchester United Ander Herrera atakuwa nje kwa Wiki 3 baada kuvunjika mfupa wa mbavuni.
Herrera, ambae alijiunga na Man United mwanzoni mwa Msimu huu akitokea Athletic Bilbao na kuifungia Bao 2 katika Mechi 4 za Ligi Kuu England, anaungana na Listi ndefu ya Majeruhi ya Timu hiyo wakiwemo Jonny Evans, Chris Smalling, Phil Jones, Jesse Lingard, Michael Carrick, Marouane Fellaini na Ashley Young.
Ingawa Carrick, Fellaini na Young wameanza tena Mazoezi hawatarajiwi kuwa fiti kwa Mechi ijayo ya Ligi Jumapili na Everton na hao wanaungana na Nahodha Wayne Rooney ambae atazikosa Mechi 3 baada ya kupewa Kadi Nyekundu walipocheza na West Ham Mechi iliyopita.
Herrera aliumia na kutolewa katika Dakika ya 74 Man United walipocheza na West Ham na awali ilidhaniwa ameumia Mgongo hadi uchunguzi wa kina ulipofanywa.
Jumapili Man United watapambana na Everton na kisha Ligi itaenda Mapumziko ya Wiki mbili kupisha Mechi za Kimataifa na baada ya hapo zitafuata Mechi za Ligi dhidi ya West Brom, Chelsea na Manchester City.
MAN UNITED - MECHI ZIJAZO
**Saa za Bongo
Oktoba 5 Saa 1400: Man United v Everton
Oktoba 20 Saa 2200: West Brom v Man United
Oktoba 26 Saa 1900: Man United v Chelsea
Novemba 2 Saa 1630: Man City v Man United
**Zote Ligi Kuu England
0 comments:
Post a Comment