KAMATI Kuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imepiga kura kuzuia umiliki wa tatu wa wachezaji ambao umekuwa ukiruhusu wawekezaji wa nje kunufaika na uhamisho.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter amesema kikosi kazi kitaandika sheria sasa ya kufuata.
Uamuzi huo wa leo ni ushindi wa kisiasa kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na Rais wake, Michel Platini, ambaye amekuwa akirudia kuitaka FIFA kuchukua hatua.
Usajili wa Manchester City wa Pauni Milioni 32 kwa Eliaquim Mangala kutoka Porto msimu huu ni moja ya mifano ya dili za umiliki wa pande tatu
Usajili wa Manchester United pia kwa beki Marcos Rojo uliripotiwa kuhusisha panda tatu za wamiliki
Umiliki wa panda tatu ni maarufu kwa mawakala, wawekezaji na klabu za Latin Amerika, Hispania na Ureno, lakini tayari umezuiwa nchini England.
Licha ya hivyo, klabu kadhaa za Ligi Kuu England zimeripotiwa kununua wachezaji kwa wamiliki wa tatu pia ili kufanikisha nyota zilizowasajili msimu huu.
Eliquim Mangala aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 32 kutoka Porto kwenda Manchester City, Marcos Rojo Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon kwenda Manchester United na Lazar Markovic Pauni Milioni 20 kutoka Benfica kwenda Liverpool wote waliripotiwa kununuliwa kwa wamiliki watatu.
UEFA inasema uhamisho wa aina hiyo unazigharimu klabu fedha nyingi wakati wa kununua wachezaji na wakati mwingine unawakwamisha wachezaji wanapotaka kununuliwa na klabu ambazo haziko tayari kulipa kwa wamiliki watatu- na haina msaada kwa mchezaji ambaye anaachwa na klabu.
0 comments:
Post a Comment