Muwezeshaji wa mafunzo ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma Lawrence Chuma
Inaelezwa kuwa chanzo cha baadhi ya viongozi wa umma kutokuwa na uhusiano mzuri na wanachi wao vijijini na kujiona ni miungu watu na kuzikalia taarifa za mapato na matumizi ni ukosefu wa ‘utawala bora’ na kutopevuka kwa demokrasia miongoni mwao.
Mtandao wa jinsia Tanzania Gender Networking Programme (TGNP) umetoa mafunzo katika ukumbi wa Coffee Garden Jijini Mbeya, kwa baadhi ya wananchi kupitia vituo vya taarifa na maarifa kutoka Kata za Tembela,Mshewe na Ijombe wakiwemo na wanahabari ili kuwajengea uwezo na ufahamu wa haki zao katika ufuatiliaji hali inayowasabaisha kupaza sauti zao kwa watendaji kuacha kuwachukulia kama wapinga maendeleo pindi wanapofuatilia taarifa za miradi yao.
Hivyo muwezashaji wa mafunzo huyo ameomba viongozi kuacha tabia ya kutokua miungu watu kwa wananchi wao katika utekelezaji wa kazi za kila siku
Sarah Jailos ni ni mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hayo ambeye pia ni Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa cha Twigushe ,Kata ya Ijombe mkoani Mbeya kumekuwa na changamoto kati yao na viongozi wao pindi wanapotaka kupata taarifa ya miradi yao, viongo hao wamekuwa wakiwaita ni wapinga maendeleo.
Aidha, Sabina Mwalyego ambaye ni Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa Kata ya Mshewe amesema changamoto kubwa alioipata ni baada ya Serikali kuwapatia fedha zaidi ya sh,mil. 31 kwaajili ya kujenga nyumba tatu za walimu ambapo mkuu wa shule hiyo alijenga nyumba moja yenye thamani ya sh, mli.5 badala ya nyumba tatu kama ilivyokusudiwa ndipo wao kama viongozi wa kituo cha taarifa na maarifa walilazimika kufuatilia kwa ukaribu ili kubaini ubadhirifu aliyoufanya mkuu huyo.
TGNP ilianza kutoa mafunzo ya dhana ya utawala bora na suala la bajeti kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini,madiwani,wanahabari na watendaji wa kata na vijiji na hatimaye kwa wananchi kupitia vituo vya taarifa na maarifa ambavyo vinafanya kazi na mtandao huo wa kijamii tangu september 16 mwaka huu, lengo likiwa kushirikishana na kujifunza umuhimu wa kufuatilia matumizi na rasilimali za umma ili kuboresha uwajibikaji,utawala bora katika ngazi hizo.
0 comments:
Post a Comment