Kikosi kizima cha Yanga kinatarajia kuondoka kesho kwenda mjini Morogoro tayari kwa mechi yake dhidi ya Mtibwa Sugar.
Yanga ambayo inaendelea na mazoezi chini ya Kocha Marcio Maximo, ipo katika hali nzuri.
Wiki iliyopita, Yanga ilionyesha kikosi chake baada ya kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii.
Yanga itafungua dimba na Mtibwa Sugar ambayo ni moja ya timu ngumu na kongwe kwenye Ligi Kuu Bara.
Kikosi kizima cha Yanga kitaondoka na basi lake aina ya Youtong kwenye mkoani humo.
Taarifa kutoka Yanga zimeeleza kila kitu kuhusiana na safari hiyo zimakamilika.
0 comments:
Post a Comment