KWA mara ya kwanza akiwa kama kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amepiga picha ya pamoja na kocha wa zamani Sir Alex Ferguson katika tukio ambalo Mdachi huyo alifichua kuwa anamwandaa Ryan Giggs kuwa mrithi wake hapo baadae.
Giggs ambaye amecheza Old Trafford kwa misimu 24, sasa ni kocha msaidizi wa Manchester United na alikuwa mgeni wa heshima kwenye hafla ya chakula cha hisani iliyofanyika Old Trafford Alhamisi jioni.
Van Gaal na Giggs wakajumuika na sura maarufu za Old Trafford wakiwemo Ferguson, Denis Law na Bryan Robson.
Louis Van Gaal, 63 akasema Giggs ni mfano mzuri kwa wachezaji na kuweka wazi kuwa msaidizi wake huyo ana vigezo vyote vya kuwa ajaye wa Manchester United. Nameongeza Giggs anafaaa kuwa kocha na kwa sasa anamuandaa kuja kuwa kocha mkuu wa timu ya Man U Kwa baadayee
0 comments:
Post a Comment