Mshambuliaji nyota wa Mbeya City Fc Paul Nonga yuko ‘fit’ tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kupigwa jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza mapema leo Nonga aliyekosa mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo dhidi ya Ruvu JKT kutokana na kuwa na kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wa mwisho msimu uliopita alisema kuwa licha ya kupata suluhu kwenye mchezo huo lakini timu ilicheza vizuri jambo ambalo linampa imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa pili ambao ataingia kuongeza nguvu.
“Tulicheza vizuri mchezo wa kwanza,binafsi nilifurahishwa na kiwango walichokionyesha wachezaji wenzangu, niko fiti tayari kuwa vaa Coastal na nina imani kubwa kuwa tutaibuka na ushindi kwa sababu timu yetu ni nzuri na ninaingia kikosini kuongeza nguvu baada ya kukosa mchezo wa kwanza kwa kadi nyekundu”. alisema Nonga.
0 comments:
Post a Comment