Mlinzi wa kutumainiwa wa kikosi cha Mbeya City Fc Deo Julius anatarajia kurejea uwanjani jumamosi hii kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kukipiga dhidi ya Coastal Union ya Tanga baada ya kuumia na kutolewa nje kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya JKT Ruvu iliyopigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mapema leo Daktari Mkuu wa timu Dr Joshua Kaseko amethibitisha kuwa mlinzi huyo sambamba na kiungo Stive Mazanda ambaye naye alipata majeraha kwenye mchezo wa huo wa kwanza wana nafasi kubwa ya kurejea uwanjani kuwakabiri ‘wagosi wa Kaya’ kutokana na hali zao kuendelea vizuri tofauti na majeruhi wengine waliopo kikosini Eric Mawala, Alex Seth na John Kabanda ambao hawataweza kabisa kuwemo kwenye kikosi cha jumamosi kutokana na hali zao kuwa hazijatengemaa.
“Deo na Mazanda hali zao zinazendelea vizuri na nina imani watakuwa wamepona na kurejea kuichezea timu kwenye mchezo wa jumamosi, lakini majeruhi wengine Seth, Mawala na kabanda hali zao bado siyo nzuri hivyo hawataweza kabisa kuwepo kwenye mechi dhidi ya Coastal Union” amesema Dr Kaseko
0 comments:
Post a Comment