Kongamano la aina hii pia ulifanyika huko Panama na Saint-Petersburg kwa Nchi Wanachama wa FIFA wa Mabara ya Amerika na Ulaya na kudhuriwa na Makocha na Maafisa wa Mabenchi ya Ufundi ya Nchi hizo.
Lengo kuu la Mikutano ya aina hii ni kujifunza mbinu za Ufundi kutoka kwenye Kombe la Dunia ili kuendeleza Soka katika ngazi zote Duniani.
Mbali ya michango ya Jopo maalum la Ufundi la FIFA, Mkuu wa Marefa wa FIFA, Massimo Busacca, na Mwakilishi kutoka, IFAB [Bodi ya Kimataifa ya Vyama vya Soka ambalo ndio Kundi waanzilishi wa Soka Duniani], Washiriki watajadili mbinu mpya za huko Brazil, mambo ya Kitaalm ya Utabibu katika Soka na matumizi ya Teknolojia Mstarini Golini na Rangi inayoyeyuka kwa ajili ya Frikiki.
Mikutano ya aina hii inatarajiwa kuhudhuriwa na Wanachama wote 209 wa FIFA.
0 comments:
Post a Comment