Dar
es Salaam. Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaonya
wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanaotishia maisha Mwenyekiti wa
Kamati ya mashindano ya imataifa wa klabu hiyo, Seif “Magari” Ahmed kuwa
sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katika
taarifa yake aliyoitoa jana, Manji amesema kuwa si suala jema kwa
wanachama kumuhusisha Seif na matokeo ya timu hiyo ambayo kwa sasa
imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja katika mzunguko wa pili
wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Manji
amesema kuwa madai kuwa Seif siyo mwanachama halali wa Yanga hayana
msingi wowote na kuyaita madai hayo kuwa ni ya uzushi na yanaenezwa na
maadui zao ambao hawaitakii Yanga mema.
Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu ambazo zimewahusisha uongozi na baadhi ya wanachama jambo ambalo si la kweli.
Alifafanua kuwa ni haki kwa kwa nia njema kwa wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi
na ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya na siyo
kumuhisha mtu kwa moja kwa moja kutokana na mtazamo hasi walionao.
“Ushindi au mwenendo mzuri wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, wachezaji,
walimu, viongozi, wanachama na wapenzi kwa ujumla. Uongozi ulikutana na
wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na
kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na
kuchukua hatua ya kubadilisha benchi la ufundi,” alisema Manji.
Aliongeza
kwa kusema kuwa uongozi ulifika mbali zaid kwa kutoa adhabu na onyo
kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi
kilichopita na kusikitishwa kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia
vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli
haupo ama kwa faida zao binafsi, au kwa kutumiwa na watu ambao hawana nia njema kwa klabu.
Manji
pia aliwaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo
kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia
sana kuzorotesha michezo nchini.
0 comments:
Post a Comment