Sophimba Mwenyekiti wa UWT Taifa
………………………………………………………………………………………………….
Na Anna Nkinda – Maelezo
Umoja
wa Wanawake wa Tanzania (UWT) umempongeza Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba linalotarajia kuanza
leo Mjini Dodoma.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya
habari na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Eva Mwingizi
ilisema uteuzi wa Rais umezingatia umri, weledi, uzoefu na uwakilishi wa
makundi mbalimbali yakijamii.
Mwingizi
alisema uteuzi huo umeangalia asilimia 50 ya uwakilishi wa wajumbe 201
hii ikiwa ni wanawake 100 na wanaume 101 pia Bunge hilo linajumuisha
wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wa Baraza la
wawakilishi Zanzibar.
Aidha
katibu Mkuu huyo alilitakia heri Bunge hilo na kuwaomba wajumbe
waliochaguliwa kutambua kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuzingatia maoni
ya wananchi ya kutengeneza katiba ya Tanzania yenye kulinda, kutetea na
kusimamia maslahi ya Taifa kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
0 comments:
Post a Comment