Ndege iliyokuwa imetekwa
Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia ndiye aliyeiteka nyara .
Maafisa mini Geneva wanasema kuwa naibu huyo wa rubani alichukua usukani wa ndege hiyo rubani wake alipokwenda msalani kwa haja.
Tukio hilo inaripotiwa kutokea ndege hiyo aina ya Boeing 767-300 ilipokuwa ikipaa katika anga ya Sudan.
Rubani huyo msaidizi alibadili mkondo wa
ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Rome Italia ,na kuipaa hadi Uswisi
alipoitua katika uwanja wa ndege wa Geneva.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote 200 wako salama (chanzo BBC Swahili).
Ripoti ya idara inayosimamia usafiri wa
ndege ya Uswisi inasema kuwa rubani huyo msaidizi aliomba uraiya kabla
ya kutua ndege hiyo na akajisalimisha kwa maafisa wa usalama waliokuwa
wameizingira ndege hiyo.
Polisi walimtia mbaroni mara moja .
0 comments:
Post a Comment