Dmytro Bulatov akiwa hospitalini kwa matibabu
Dmytro Bulatov kabla ya kujeruhiwa akiwa katika harakati zake za kisiasa
Dmytro Bulatov alionekana kwenye
runinga juma lililopita sikio lake likiwa limekatwa na akiwa na jeraha
usoni, akadai kuwa alitekwa na watu asio wajua na kuteswa kwa siku nane .
Hali yake iliibua hamaki miongoni mwa maelfu ya waandamanaji wanaomtaka rais Viktor Yanukovych ajiuzulu.
Yamkini
Bulatov ni mmoja kati ya kundi la wamiliki wa magari wa AutoMaidan
wanaokisiwa kuhusika na maandamano yanayoendelea katika ukumbi mkubwa wa
Maidan square jijini Kiev.
Kiongozi wa upinzani Vitali Klitschko
alisema viongozi wa muungano wa Ulaya ndio waliofanikisha matibabu ya
Bulatov nje ya Ukraine baada ya kusikia kuwa aliteswa na watekaji wake .
Serikali inadaiwa ilituma maafisa wake kumkamata akiwa amelazwa Hospitalini lakini wafuasi wake wakawazuia.
Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Ukraine
Leonid Kozharahata amepuuzilia mbali madai ya kutekwa na kuteswa kwake
akisema ni uwongo mtupu
0 comments:
Post a Comment