Wednesday, 22 January 2014

WATU 1500 WAPEWA ELIMU YA KUPAMBANA NA MAGONJWA MBALIMBALI


images
Na Gladness Mushi  Arusha
……………………………………………
Zaidi ya watu 1500 kutoka katika maeneo mbalimbali ndani ya mji wa
Arusha wamefanikiwa kupewa elimu ya jinsi ya kupambana na magonjwa

mbalimbali ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha umaskini kwenye mji wa

Arusha
Aidha elimu hiyo pia iliweza kwenda sanjari na jinsi ya kupambana nayo
hasa kwa magonjwa ambayo yamekuwa ni kikwazo zaidi kwenye maisha ya

kila siku.
Elimu hiyo imetolewa na kanisa la T.A.G God Glory Temple lililopo
maeneo ya JR jijini Arusha ambapo kanisa hilo limedai kuwa huo ni

mkakati wa kuwasaidia jamii kwa kutoa elimu mbalimbali kwa
kushirikiana na wataalamu mbalimbali
Akiomngea na “FULLSHANGWE”mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Gremas Simbani
alidai kuwa  watu hao waliweza kupewa elimu dhidi ya magonjwa

mbalimbali kwa kipindi cha mwaka jana
Simbani alisema kuwa uchunguzi uliofanywa na kanisa hilo umeweza
kubaini kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanakabiliwa na changamoto

ya magonjwa hali ambayo inasababisha mambo mbalimbali kukwama na

badala yake lawama kuwa nyingi
Alifafanua kwa kusema kuwa mambo hayo ambayo yanazaliwa na magonjwa ya
kila siku ni pamoja na umaskini ambao umekithiri sana kwennye maisha

ya kila siku, vifo ambavyo havina umuhimu, pamoja na matatizo kama

vile lawama,malalamishi ambayo nayo huchonganisha hata vichwa vya

baadhi ya viongozi.
“tuna mikakati ya kuhakikisha kuwa mbali na kuweza kusaidia serikali
lakini pia tunasaidia hata jamii kwani kwa kuachia serikali pekee bado

shida itakuwepo sana kwenye maisha ya watanzania na baada ya kuweza

kutoa elimu ya kupambana na magonjwa sasa tutaangalia na kufanya

tathimini imewasaidia watu kwa jinsi gani”aliongeza Simbani
Wakati huo huo alizitaka nazo taasisi mbalimbali za dini kuhakikisha
kuwa zinaweka utararibu wa kuangalia namna ya kusaidia Serikali hasa

kwa kutoa elimu mbalimbali ambazo zitalenga kuwasaidia watanzania

kwani taasisi hizo zina uwezo wa kuwafikia wengi zaidi kuliko taasisi

nyingine zozote
Alisema kuwa kwa kufanya hivyo kutaweza kuraisisha malengo na sera
mbalimbali ambazo zimewekwa na serikali hasa zile za kupambana na

umaskini kwani kwa sasa baadhi ya sera wakati mwingine zinashindwa

kutekelezwa kutokana na kuwa hakunaa ushirikiano

Related Posts:

0 comments: