Mwandishi
,Dominic
Joseph Maro Tanga
HALMASHAURI ya jiji la Tanga
inatarajia kutumia kiasi cha sh, 4.5 bilioni ktk kipindi cha mwaka wa fedha wa
2014/15 kwaajili ya kuendesha mradi wa kupeleka maji safi ya bomba ktk vijijini
10.
Meya wa jiji la Tanga Omari Guledi amesema kuwa ktk kipindi hicho
Halmashauli ya jiji la Tanga imepanga kufikisha maji safi ya bomba ktk vijiji
10 vilivyo ktk upande wa kaskazini na magharibi ya wilaya ya Tanga.
Amevitaja
vijiji hivyo vitakavyonufaika na mradi huo
kuwa ni pamoja na Chongoleani, Ndaoya, Kibafuta, Mleni, Mpirani,
Marungu, Geza, Mapojoni Mwarongo na Kirare.
Guledi
amesema kuwa mradi huo wa kupeleka maji ktk vijiji hivyo unakuja kufuatia jiji
la Tanga kujitosheleza kwa usambazaji maji kwa wananchi wake wa mjini kwa
kiwango kikubwa ambapo ametanabaisha kuwa kwa sasa nguvu zinaelekezwa kwa
wananchi walio vijijini
0 comments:
Post a Comment