Wednesday, 22 January 2014

KIFO CHA MBUNGE WA CHALINZE AFARIKI DUNIA RAMADHANI BWANAMDOGO CHA ZUA MAJONZI KWA WANA CCM

 Mbunge  wa  jimbo la Chalinze Ramadhan Bwanamdogo pichani  kushoto akizungumza na wapiga kura  wake enzi za uhai  wake
Taarifa  ambazo  mtandao  huu    umezifikia  zinadai  kuwa aliyekuwa Mbunge  wa  jimbo la Chalinze Ramadhan Bwanamdogo ambae  alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa  jijini Dar es Salaam  amefariki  dunia .

Mbunge  huyo amefariki  leo  asubuhi  akiwa katika Hospitali  hiyo akiendelea  kupatiwa matibabu  baada ya  kulazwa  kwa  zaidi ya  wiki  moja  sasa .


Kifo cha mbunge  huyo kimekuja  huku  watanzania wakiwa bado katika simanzi  za  kifo cha aliyekuwa waziri  wa  fedha  na  mbunge wa  jimbo la Kalenga Iringa  kupitia  (CCM) Dr Wiliam Mgimwa na  kuendelea  kuacha pigo ndani ya chama hicho hivyo hadi sasa ni kwa kipindi cha mwaka huu  pekee ni  wabunge  wawili wa CCM wamepoteza maisha na kufanya majimbo mawili kwa  mwaka huu kubaki  wazi.
Badhii ya wanachama wa chama cha mapinduzi wamesema kua wameondokewa na mtu muhimu sana hata hivyo taarifa ya kifo cha mbunge huyo umekipokea kwa majonzi makubwa
 .........Habari  zaidi  tutaendelea  kukuletea  hapa....................
 

Related Posts:

0 comments: