Dodoma.
Jukwaa la Katiba
Tanzania (Jukata), limechagua wawakilishi 40 kutoka mitandao ya asasi za
kiraia nchini (Azaki), ambao majina yao yatapelekwa kwa Rais Jakaya
Kikwete kwa ajili ya uteuzi wa wabunge 20 wa Bunge Maalumu la Katiba.
Asasi za kiraia nchini zimepewa nafasi 20 za uwakilishi katika bunge hilo, ambalo linatarajiwa kuanza Februari mwakani.
Katika uchaguzi huo uliomalizika juzi saa 4:00
usiku, zaidi ya wagombea 100 walijinadi na kupigiwa kura na wawakilishi
wa Azaki kutoka mikoa 30 nchini.
Wapiga kura hao ni wawakilishi wa mitandao ya
Azaki wa wilaya 140, mikoa 30 na kisekta 20. Wawakilishi hao
walichaguliwa kwa kufuata uwiano wa kikanda na uwakilishi wa kisekta.
Waliochaguliwa kuwakilisha sekta ya Utawala Bora
na Uwajibikaji ni; Alban Marcossy (104) na Renatus Mkinga (78). Sekta ya
Haki za Watoto, Seif Mahumbi na James Marenya kila mmoja alipata kura
47.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Deus Kibamba aliwataja
waliochaguliwa Sekta ya Uchumi na Maendeleo, ni Martina Kabisan na
Gerald Ruhere.
Habari ni Mwandishi wa Kampuni ya New Habari 2006,
Arodia Peter na Burhan Yakub wa Kampuni ya Mwananchi Communications
(MCL). Wazee ni Charles Lwabulala na Dk Joseph Saqware.
Alitaja sekta nyingine ni vijana, Violet Edwin na
Jafari Yusuf, huku Sheria na Haki za Binadamu wakichaguliwa Sarah
Malingingwa na Elias Mathibya.
Sekta ya Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, ni Alex
Margery na Elita Chusi kila mmoja alipata kura 72. Sekta ya Jamii ni
Happiness Sengi na Dk Peter Bujari, wakati Mazingira na Maliasili ni
Magreth Katanga (56) na Jecha Jecha. Jinsia na Wanawake ni Gemma
Akilimali na Grace Mkumbwa.
Uwakilishi wa kikanda Kanda ya Kati ni Maliki
Marupu na Maendeleo Makoye; Kaskazini ni Petro Ahham na Saumu Swai;
Magharibi ni Babyegeya Bitegeko na Bihaga Simon na Kusini ni Michael
Malucha na Sharif Kombo.
Pemba ni Mussa Kombo Mussa na Fakih Hamad Ally; Juu Kusini ni Paul Kita na Raphael Mtitu.
Kanda ya Ziwa ni Mariam Mkaka na Nicas Nibengo;
Unguja ni Hassan Khamis Juma na Hafidhi Hamid Soud na Pwani ni Shaib
Lipwata na Sofia Mwakagenza.
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment