Mada ya usajili kwa watoto wanaozaliwa imekuwa muhimu
kufuatia ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,
UNICEF ya kwamba watoto Milioni 230 duniani kote hawajasajiliwa popote.
Sababu zimetajwa kuwa ni pamoja na ukosefu wa mfumo wa kuhakikisha mtoto
anapozaliwa anasajiliwa na kupatiwa cheti cha kuzaliwa. Sababu nyingine
ni uhusiano wa kijinsia ambapo wanawake ambao wanakuwa wanalea ujauzito
peke yao baada ya kukataliwa na waume zao wanashindwa kusajili watoto
wao kwani hawezi kutumia jina la ukoo wake. Nchini Tanzania yaelezwa
kuwa hatua zimechukuliwa kuhakikisha watoto wanasajiliwa ili waweze
kupata haki zao za msingi kwa usahihi.
Je hali ikoje? Basi ungana na
Tamimu Adamu wa Radio washirika Jogoo FM kutoka Ruvuma nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment