Dar na Bagamoyo.Wachumi
mbalimbali wamebashiri kuibuka kwa mfumuko wa bei wa vitu mbalimbali,
kutokana na kupanda kwa bei ya umeme inayoanza leo.
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema bei ya umeme itapanda kulingana na matumizi kuanzia leo.
Wataalamu wa uchumi waliokutana mjini Bagamoyo,
Pwani, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania kwa
mwaka 2014 unaoanza leo ikiwamo upandaji bei ya umeme.
Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Profesa Humphrey Moshi alisema ongezeko la bei ya umeme linaweza
kuchangia kwa kiwango kikubwa mfumko wa bei.
Profesa Mushi alisema kupanda kwa gharama hizo ni
kutokana na shughuli nyingi za uzalishaji kutegemea umeme, hivyo
wazalishaji watapandisha bei za bidhaa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati
(Ewura), Haruna Masebu inasema baada ya uchambuzi wa kina ilijiridhisha
maombi ya kurekebisha bei na gharama mbalimbali za Tanesco ni sahihi.
Na Elizabeth Edward na Beatrice Moses, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment