.
Jina lake ni Emmanuel Msuya ambae usiku wa November 30 2014 Escape
One Mikocheni Dar es salaam alitangazwa mshindi wa BSS kwa mwaka 2013 na
kuzichukua MILIONI 50 kutokana na matokeo kamili ya mizani hiyo ya
vipaji vya muziki kwa wachanga.
Unaambiwa kabla ya hapo, Msuya hakuwahi kushika au kumiliki zaidi ya
shilingi laki tano… yani aliwahi kupata shilingi laki tano mara moja tu
siku alipolipwa pesa ya miezi mitatu iliyotokana na mkataba wa
kuifundisha na kuisimamia Kwaya ya KKKT kucheza ili ikafanye video.
Mambo matatu makubwa aliyoyafanya kwa hizi milioni 50 za ushindi wa BSS….
Msuya amenunua nyumba ya milioni 17 nyumbani kwao Musoma mjini kama
unavyoiona hapa chini kwenye picha, amenunua hili gari lenye thamani ya
milioni 9, amejenga studio hiyo hapo juu kwenye picha ambayo imegharimu
milioni 12 na tayari ameshapata nyumba ya kufanyia biashara ya
Stationary Musoma Mjini.
0 comments:
Post a Comment