Kama umewahi kuitazama Isidingo, huyu ndio mwigizaji wao aliefariki jana
Taarifa iliyotolewa inasema kaka mtu ndio alimkuta Letty akiwa
amefariki nyumbani kwake saa tano asubuhi January 20 2014 ambapo kifo
chake kilithibitishwa saa kadhaa baadae.
Mwaka
2011 mwishoni Motsepe alitangaza hadharani kuwa amekua akiishi na
virusi vya ukimwi kwa karibu miaka 13 na uamuzi huo wa kujitangaza
alitaka kuleta mabadiliko na kuwasaidia wale wanaoishi kwenye aina hiyo
ya maisha kama yake.
Pamoja na kwamba alijitangaza kuishi na virusi vya ukimwi, chanzo cha kifo chake hakijatangazwa bado.
0 comments:
Post a Comment