REKODI ya kutofungwa ya Barcelona usiku huu imekomea
kwenye mechi ya 31, baada ya kufungwa mabao 3-2
na Valencia.
Mabao ya Barca yalifungwa na Alexis dakika ya saba na Messi
kwa penalti dakika ya 51, wakati mabao ya Valencia
yalifungwa na Parejo dakika ya 44, Piatti dakika ya 46
na Alcacer dakika ya 58.
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini bila shaka
aliuangalia mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana
Februaryi 18 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matokeo hayo yanatoa nafasi kwa Barca kuipisha
Real Madrid kileleni, kwani inabaki na pointi zake 54 sawa
na Atletico Madrid, ikiwa imecheza mechi moja zaidi.
Real ina pointi 53 na imecheza mechi 21, wakati Barca 22.
0 comments:
Post a Comment